Kituo hicho katika mkoa wa Hudaydah kilipigwa angalau mara mbili usiku wa Alkhamisi, ambapo shambulio la pili lilijiri wakati vikosi vya ulinzi wa raia na uokoaji vilikuwa vikizima moto na kuwaokoa manusura. Shambulio hilo la pili liliua takriban wahudumu watano.
Kituo cha Habari cha Palestina na Televisheni ya al-Manar zimeripoti kuwa, watu wasipongua 33 wameuawa katika shambulio hilo, huku wengine zaidi ya 80 wakijeruhiwa.
Serikali ya Yemen imelaani shambulizi hilo na kusema ni jinai ya wazi ya kivita yenye lengo la kuunga mkono utawala wa Kizayuni na kuuwezesha kuendelea na mauaji ya kimbari ya Gaza.
Imeeleza bayana kuwa, mashambulizi hayo yanathibitisha kuwa Marekani inashambulia kwa makusudi miundombinu ya raia nchini Yemen kwa kutumia visingizio na sababu za uongo.
Serikali ya Yemen imeapa kwamba, uhalifu huu hautapita bila kujibiwa, ikisisitiza kuwa Marekani haitaambulia chochote ila kushindwa na kufeli kwa fedheha. Jeshi la Marekani limedai kuwa bandari hiyo ni chanzo cha mafuta kwa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah.
Majimbo ya Sana'a, al-Bayda na Hudaydah pia yalikumbwa na mashambulizi hayo. Marekani imezidisha mashambulizi yake mabaya dhidi ya nchi hiyo maskini tangu mwezi uliopita, kwa amri ya moja kwa moja ya Rais Donald Trump.
342/
Your Comment